• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 20 wamekufa katika tukio la kukanyagana kwenye misa Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-02-02 19:16:57

    Polisi nchini Tanzania wamesema waamini 20 wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana katika misa iliyoendeshwa jana jioni kwenye uwanja wa mpira mjini Moshi.

    Watu hao walikusanyika uwanjani hapo kusubiri kupakwa mafuta ya upako kutoka kwa mchungaji Bonface Mwamposa.

    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Moshi Bw. Salum Hamduni amesema tukio hilo lilitokea kati ya saa moja na nusu hadi saa mbili jioni, wakati watu wakisongamana milangoni mafuta hayo yalipowekwa.

    Watu saba wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, na Bw. Hamduni amemtaka Mchungaji Mwamposa ajisalimishe polisi kuhojiwa.

    Mchungaji Mwamposa amekuwa akifanya mahubiri katika nchi nzima, lakini zaidi mjini Dar es salaam, na kuvutia watu wengi wanaoamini kuwa mafuta yake ya upako yanatibu magonjwa na kuleta neema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako