• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yakamata wahamiaji 71 haramu kutoka nchi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2020-02-03 08:53:24

    Wahamiaji 71 haramu kutoka nchi mbalimbali wamekamatwa na mamlaka ya uhamiaji ya Tanzania.

    Mkuu wa idara ya uhamiaji ya mkoa wa Mbeya Bw. Shaaban Hatibu, amesema wahamiaji hao wamekuwa wakifanya kazi katika mkoa wa Mbeya bila vibali vya ukazi na kazi. Bw. Hatibu pia amesema, watanzania sita pia wamekamatwa kutokana na kusaidia wahamiaji kuingia nchi hiyo bila ya ruhusa.

    Amesema baadhi ya wahamiaji haramu waliokamatwa watarudishwa kwenye nchi zao, wengine watatozwa faini, na wengine watafikishwa mahakamani kwa kosa la ukazi haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako