• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Novak Djokovic na Sofia Kenin waondoka na taji la Grand Slam kwa wanaume na wanawake

  (GMT+08:00) 2020-02-03 10:35:36

  Novak Djokovic jana alifanikiwa kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Australia kwa kushinda taji la 17 la Grand Slam baada ya kumnyuka Dominic Thiem kwenye seti tano za fainali. Mserbia huyo ameshinda 6-4 4-6 2-6 6-3 6-4 katika uwanja wa Melbourne Park. Djokovic, mwenye miaka 32, alimwita dokta mara mbili kiwanjani kabla ya kujikaza na kupambana kiume. Kwa upande wake Thiem, Muastralia mwenye miaka 26, bado anasubiri taji lake kubwa baada ya kushindwa kwenye fainali ya Grand Slam. Kwa upande wa akina dada kwenye fainali zilizofanyika Jumamosi Mmarekani Sofia Kenin amefunga michuano hiyo kwa kuondoka na taji la Grand Slam. Kenini alimshinda Garbine Muguruza kwa 4-6 6-2 6-2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako