• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masaibu ya Wanyama katika klabu ya Spurs huenda yakapelekea mkataba wake kuvunjwa

  (GMT+08:00) 2020-02-03 16:36:07

  Huenda klabu ya Ligi Kuu Uingerza, Tottenham Hotspur ikatengana na Mkenya Victor Wanyama licha ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho hivi karibuni bila ya mchezaji huyo kuondoka jijini London. Wanyama amekuwa mzigo kwa klabu hiyo na bado hajashiriki mechi yoyote ya klabu yake mwaka huu. Spurs walikuwa na hamu kubwa ya kumuuza kiungo huyo wakati wa dirisha la uhamisho la Januari lakini wanunuzi wakiwemo Lazio na Celtic walikimbizwa na bei ya KSh 1.3 bilioni iliyokuwa ikiitishwa na Spurs. Vyombo kadhaa vya habari kwa sasa vinaripoti kuwa mawakala wa Wanyama wanafanya mazungumzo kuhusu kukatiza mkatba wake ili kumruhusu kuondoka akiwa huru. Wanyama amesalia na miezi 18 katika mkataba wake na Spurs na pia vilabu vinavyomvizia vina shaka na mshahara wake mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako