• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazingatia hatua za kusaidia kampuni zinazofanya biashara ya nje

    (GMT+08:00) 2020-02-03 18:10:11

    Wizara ya biashara ya China jana imesema, kampuni zinazoshughulikia biashara ya nje zitaanza tena uzalishaji na usafirishaji bidhaa baada ya tarehe 8 mwezi huu, ambayo ni siku ya mwisho wa sherehe za mwaka mpya wa Kichina, na mamlaka husika zinaharakisha juhudi za kuboresha mazingira ya biashara na kupunguza mizigo yao.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bingnan amesema, idara na serikali za mitaani za ngazi mbalimbai zinatunga sera za makini ili kuweka mazingira mazuri ya biashara, na kupunguza mizigo ya kampuni.

    Pia amesema, wizara hiyo inafutailia kwa makini mlipuko wa virusi vya korona nchini China. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipongeza China kutokana na juhudi zake katika kukinga na kudhibiti mlipuko huo, na haikupendekeza kuweka vikwazo dhidi ya biashara na usafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako