• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa amani ya Mashariki ya Kati wa Trump ni changamoto kwa mipaka ya kimataifa iliyokubaliwa

    (GMT+08:00) 2020-02-03 20:42:19

    Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera ya diplomasia na usalama Bw. Josep Borrell amesema mpango mpya wa amani ya Mashariki ya Kati uliotolewa na Marekani unaleta changamoto kubwa kwa mipaka ya kimataifa iliyokubaliwa.

    Baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Jordan Bw. Ayman Safadi, Bw. Borrell amesema Umoja wa Ulaya na Jordan zote zinaunga mkono mpango wa nchi mbili na kuheshimu sheria za kimataifa.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana tarehe 10 mwezi huu ili kujadili mpango huo uliotolewa na Marekani, na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina na balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Danny Danon watahudhuria mkutano huo. Palestina inaandaa azimio la kulaani mpango huo wenye utata ingawa huenda azimio hilo likakataliwa na Marekani

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako