• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA: Dereva wa Red Bull Verstappen atamba kumshinda Lewis Hamilton kwenye mbio za ubingwa wa dunia mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-02-04 07:48:28

  Dereva wa Red Bull Max Verstappen amesema anaweza kumshinda Lewis Hamilton kwenye mbio za ubingwa wa dunia za mwaka huu kama gari yake itakuwa nzuri. Mholanzi huyo mwenye miaka 22 anaona timu yake inaweza kuongeza changamoto kwenye timu ya Mercedes. Amesisitiza kuwa Lewis ana uwezo mkubwa lakini yeye sio Mungu. Verstappen anaamini kwamba Hamilton na Mercedes wanaweza kushindwa kama Red Bull itawapa shinikizo kubwa. Mwaka jana Hamilton alikiri kwamba alimpa Verstappen nafasi Zaidi wakati walipokuwa wanakimbizana kwa karibu kwasababu ya sifa ya mholanzi huyo ya kuendesha kwa fujo. Lakini Verstappen alisema kwamba yeye haamini hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako