• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani ya kushinda vita dhidi ya virusi vya korona kutokana na nguvu bora ya kimfumo

    (GMT+08:00) 2020-02-04 09:17:21

    Kamati ya kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China jana Jumatatu ilifanya mkutano, ikisikiliza ripoti kuhusu kazi za udhibiti wa mlipuko wa virusi vya korona zilizotolewa na timu ya uongozi wa kazi hizo na idara husika. Rais Xi Jinping aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

    Mkutano huo umeainisha kuwa, mlipuko huo wa virusi vya korona ni kama mtihani mkubwa kwa mfumo na uwezo wa usimamizi wa China. Hivi sasa vipaumbele vya kazi ni kufanya juhudi zote kuwatibu wagonjwa, kuhakikisha ugavi wa raslimali za kimatibabu, na kujitahidi kuongeza kiwango cha wagonjwa kupewa matibabu na kupona, na kupunguza kiwango cha maambukizi na vifo. Wakati huohuo, mkutano huo umeagiza kuhakikisha utoaji wa bidhaa za mahitaji ya maisha kama vile mboga, nyama, maziwa, mayai na nafaka, na kuimarisha usafirishaji, usambazaji na upatikanaji wa bidhaa hizo sokoni.

    Mapema siku hiyo, ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China ilifanya mkutano na wanahabari, ikisema kwa ujumla suala la upungufu wa raslimali za kimatibabu katika mkoa wa Hubei unaoathiriwa zaidi na mlipuko wa virusi vya korona, "limetatuliwa kwa kiasi kikubwa", na ugavi wa raslimali za kimatibabu katika nchi nzima umefikia uwiano.

    Ni dhahiri kuwa nguvu bora ya kimfumo wa ujamaa wenye umaalum wa kichina inaendelea kubadilika kuwa ufanisi wa usimamizi, na inaendelea kutatua masuala na changamoto wakati mikakati na maamuzi yanapotekelezwa, hali ambayo inafanikisha hatua kwa hatua juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako