• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Madaktari na wauguzi zaidi ya 8000 wakusanyika mkoani Hubei kushiriki mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona

  (GMT+08:00) 2020-02-04 18:03:45

  Hadi kufikia saa mbili usiku wa tarehe 2, zaidi ya wahudumu 8000 wa afya kutoka sehemu mbalimbali za China na jeshi la China wamekusanyika mkoani Hubei, China wakisaidia mkoa huo ulioko mstari wa kwanza katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vipya vya korana. Jana usiku, hospitali ya Huoshenshan iliyojengwa hivi karibuni ilianza kuwapokea wagonjwa walioambukizwa virusi vya korona.

  Mtaalamu wa Kamati ya Afya ya China Bi. Li Lanjuan jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kazi ya kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korana itapata mafanikio. Anasema,

  "Hivi sasa vikosi vingi vya matibabu kutoka sehemu mbalimbali vimefika hapa, ambavyo vina nguvu kubwa. Mfano mkoa wa Zhejiang umetuma wahudumu 330 wa afya. Kwa kupitia uungaji mkono kutoka pande, upangaji mbalimbali mzuri wa wahudumu wa afya wa Wuhan, kuongeza nguvu ya matibabu, na kuimarisha uokoaji na matibabu kwa wagonjwa walioathirika vibaya, hali itadhibitiwa vizuri, na pia tunaweza kupunguza kiwango cha vifo vinavyotokana na virusi hivyo. "

  Baada ya kukamilika kwa ujenzi na maandalizi ya awali, hospitali ya Huoshenshan ya Wuhan iko tayari kuanza kutumika. Jeshi la China limetuma wahudumu 1,400 wa afya watakaokuwa na jukumu la uokoaji na matibabu. Mkurugnezi wa chumba cha dawa cha hospitali hiyo Bw. Ji Bo anasema,

  "Hivi sasa tuna dawa aina zote za kuokoa na kutibu nimonia, zikiwemo dawa za kukinga maambukizi, dawa za kupambana na virusi, na dawa za uokaoji wa dharura. Dawa hizo zinaweza kutolewa na kutumiwa wakati wowote. Tuko tayari saa 24 kwa siku. "

  Jana usiku, hospitali hiyo yenye vitanda 1000 ilianza kuwapokea wagonjwa 50 kutoka hospitali nyingine mjini Wuhan. Bi. Li Lanjuan alisema, kutokana na uzinduzi rasmi wa hospitali hiyo, na hospitali nyingine ya Leishenshan itakayozinduliwa baadaye wiki hii, suala la kuwakusanya wagonjwa wa virusi vipya vya korana ili wapewe matibabu kwa pamoja litatatuliwa kwa ufanisi zaidi. Anasema,

  "Baada ya kuzinduliwa kwa hospitali hizo mbili, shinikizo kwa Wuhan litapungua kwa kiasi kikubwa. Watu wengi zaidi wanaweza kutengwa na kutibiwa. Nguvu za hospitali nyingine pia zimeimarishwa. Tuna matumaini kuwa suala la kupata tiba hospitalini kwa wagonjwa linatatuliwa vizuri kwa kupitia ushirikiano na juhudi za pamoja. "  

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako