• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano ya kikabila yasababisha vifo vya watu 20 kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2020-02-04 18:58:18

    Watu 20 wameuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika mapigano makali ya kikabila katika mkoa wa Lower Juba, kusini mwa Somalia.

    Waziri wa habari wa Jubbaland Bw. Abdi Hussein Ahmed amesema mapigano hayo yalitokea siku tatu zilizopita katika wilaya ya Kismayo kati ya makabila mawili kutokana na migogoro ya ardhi na yalianza tena leo asubuhi.

    Bw. Ahmed ameongeza kuwa, utawala wa Jubbaland unajaribu kumaliza mapigano hayo, lakini juhudi bado hazijafanikiwa, pia aliwashtumu wapiganaji wa kundi la al-Shabab wanaokalia eneo hilo kwa kuchochea mapigano kati ya makabila hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako