• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuendelea kuvutia wawekezaji

    (GMT+08:00) 2020-02-04 19:16:09
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angella Kairuki, ameliambia Bunge kuwa serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika maeneo yote yenye rasilimali.

    Kairuki alisema kwamba serikali inaendelea kutafuta wawekezaji ili kuinua uchumi wa taifa. Alidokeza kuwa azma ya serikali ya awamu ya Tano ni kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

    Akiongea bungeni jana, Waziri Kairuki alisema kwamba lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje katika maeneo yote yenye rasilimali zinazoipa Tanzania faida ya ushindani itaendelea kuvutia wawekezaji.

    Alizitaka wizara, taasisi za serikali na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kusimamia mikakati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji katika maeneo yao ikiwamo kuainisha na kuyapembua kiyakinifu maeneo yote yenye rasilimali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako