• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vizingiti kwa ulipaji wa huduma Rwanda bila kutumia pesa taslimu

    (GMT+08:00) 2020-02-04 19:16:44
    Serikali ya Rwanda inazidi kuwahimiza raia wake kulipia huduma zao ka kutumia njia za kadi au malipo kwa njia ya simu badala ya pesa taslimu. Hili limekumbatiwa katika maeneo mengi ila kuna baadhi ya sekta ambazo zinakumbwa na ugumu wa kulipia kwa kutumia simu au kadi.

    Baadhi ya sekta hizo ni maegesho ya magari haswa nje ya maduka ya jumla, ulipaji karo ya shule, hapa shule za mashinani zikiathirika pakubwa. Sekta nyingine ni wauzaji bidhaa reja reja, makanisani na maeneo ya vyakula. Licha ya ugumu unaoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo haya, serikali imezidi kuwaraia Warwanda kukumbatia mfumo wa kulipia bidhaa na huduma pasipo kutumia pesa taslimu ila kwa malipo ya simu au kadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako