• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ataka ushindi katika vita dhidi ya virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-02-04 21:19:47

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amezitaka kamati za ngazi mbalimbali za Chama na serikali kutoa kipaumbele kwa kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona na kushinda vita hivyo.

    Bw. Li amesema hayo kwenye mkutano wa tume ya uongozi wa kazi ya kupambana na virusi vya korona uliofanyika hii leo hapa Beijing.

    Mkutano huo umesisitiza kuwa, mkoa wa Hubei, haswa mji wa Wuhan bado ni muhimu zaidi katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, kulinda usalama wa maisha na afya ya watu ni jukumu la kwanza, kujitahidi kuongeza kiwango cha kupokea na kutibu wagonjwa, na kupunguza kiwango cha maambukizi na vifo. Mkutano huo pia umesema ni lazima kuhakikisha vifaa vya matibabu vinapelekwa na kutumiwa katika mstari wa mbele wa kupambana na virusi, na pia kuhakikisha mahitaji ya kila siku yanapatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako