• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mahakama ya Korea Kusini yamwamuru promota kuwalipa fidia mashabiki kwa Ronaldo kutocheza mechi

    (GMT+08:00) 2020-02-05 07:35:51

    Mahakama ya Korea Kusini imemuamuru promota wa nchi hiyo kuwalipa fidia mashabiki, kwa Cristiano Ronaldo kutoonekana kiwanjani kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Seoul Julai mwaka jana. Nyota huyo wa Juventus alikaa kwenye benchi hadi mechi inamalizika ambayo walitoka sare ya 3-3 na timu ya K-League all-stars licha ya mashabiki wapatao 65,000 kumshangilia. Promota wa mechi The Festa alitoa matangazo mengi akimpigia debe mshambuliaji huyo wa Ureno. Bei ya tiketi ilikuwa kutoka won 30,000 sawa na dola 25 hadi won 400,000 ambazo zote ziliuzwa chini ya dakika tatu, wengi wakiwa na hamu ya kumuona nyota huyo mwenye miaka 34 akicheza kiwanjani. Mashabiki wawili waliishtaki The Festa, kwa kuishutumu kutoa matangazo ya uongo, na mahakama ya wilaya ya Incheon imemhukumu promota kumlipa kila shabiki won 371,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako