• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya uongozi ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona yasisitiza kuinua kiwango cha kuwapokea na kuwatibu wagonjwa

    (GMT+08:00) 2020-02-05 09:07:25

    Mkutano wa timu ya uongozi ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona uliofanyika jana Jumanne ukiongozwa na waziri mkuu Bw. Li Keqiang, umeainisha kuwa mkoa wa Hubei, hasa mji wa Wuhan, bado ni eneo la kipaumbele kwenye juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi hivyo kote nchini, na kuagiza kuinua kiwango cha kuwapokea na kuwatibu wagonjwa, na kupunguza kiwango cha maambukizi na vifo.

    Mkutano huo umeamua kutuma hospitali za kuhamishika pamoja na madaktari na wauguzi elfu mbili mkoani Hubei, na kutumia mahoteli, viwanja vya michezo na vituo vya mafunzo kama vituo vya kuwapokea watu wanaoshukiwa kuambukizwa virusi hivyo, wagonjwa wenye dilili ndogo, na wale walio chini ya uangalizi wa kimatibabu.

    Habari nyingine zinasema mamlaka ya ukaguzi wa nidhamu imeanza uchunguzi na kuchukua hatua madhubuti za kuwashughulikia maofisa wasio na sifa na waliozembea katika kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona aina ya 2019-nCoV.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako