• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wawili wakamatwa kwa kukutwa na gramu 500 za herion Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-02-05 09:15:38

    Idara ya kupambana na dawa za kulevya ya Tanzania inawashikilia watuhumiwa wawili kwa kosa la kukutwa na gramu 508.163 za dawa za kulevya aina ya heroin.

    Kamishna mkuu wa Idara ya kupambana na dawa za kulevya ya Tanzania (DCEA) Bw. James Kaji amesema watuhumiwa wote ni wakazi wa mji wa Dar es salaam, na walikamatwa kwenye operesheni maalum iliyofanyika januari 27, ambapo pia walikamata nyaraka muhimu.

    Akiongea na wanahabari mjini Dar es salaam, Bw. Kaji amesema kukamatwa kwa watu hao kunafuatia taarifa za kiintelijensia kuhusiana ufuatiliaji wa biashara ya dawa za kulevya mjini Dar es salaam. Amesema watuhumiwa wawili watafikishwa mahakamani, lakini wengine wawili walifanikiwa kutoroka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako