Timu ya voliboli ya wanawake ya Kenya, KCB inapania kushinda taji la Klabu Bingwa Afrika (CAVB) mwaka huu. Warembo hao wanalenga kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu 2006 waliposhinda taji hilo. Kocha mkuu wa timu hiyo, Japheth Munala amesema wamo mbioni kuunda timu imara ili kutoa upinzani mkali katika ligi ya KVF pia mashindano mengine barani Afrika. Tangu kumalizika kwa mechi za ligi msimu uliopita, uongozi wa wanabenki hao umekuwa mbioni kutafuta wachezaji wazoefu ili kujiweka vizuri kukabili wapinzani wengine muhula huu. KCB iliyomaliza ya pili katika fainali za ligi msimu uliopita imesaini wachezaji sita wapya ambao ni kati ya mastaa wanaocheza katika timu ya taifa maarufu Malkia Strikers.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |