• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump ajigamba mafanikio ya kiuchumi wakati uchumi ukishuka

    (GMT+08:00) 2020-02-05 18:51:47

    Wakati kasi ya ukuaji wa uchumi wa Marekani ikishuka, Rais wa nchi hiyo Donald Trump jana usiku alipotoa hotuba ya tatu ya hali ya taifa ya Marekani, alisifu mafanikio makubwa ya kiuchumi ya nchi hiyo, huku akisisitiza ongezeko la ajira na maendeleo ya biashara.

    Katika hotuba yake, rais Trump amesema, serikali yake imesahihisha sera za kiuchumi zilizoshindwa za serikali iliyopita, na kufufua uchumi wa Marekani kwa kuondoa sheria, kupunguza ushuru, na kufikia makubaliano ya haki na kunufaishana ya biashara.

    Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na wizara ya biashara ya Marekani, ongezeko la uchumi wa nchi hiyo lilishuka hadi asilimia 2.3 mwaka jana kutoka asilimia 2.9 ya mwaka 2018, takwimu ambazo zinaonyesha kupungua kwa uwekezaji wa kibiashara na matumizi katika mahitaji ya kila siku, pamoja na kudidimia kwa usafirishaji bidhaa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako