• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara watakiwa kutoingiza mayai kutoka nje

    (GMT+08:00) 2020-02-05 19:27:05
    Wafanyabiashara wa mayai wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania wametakiwa kuacha tabia ya kuendelea kuagiza na kuingiza mayai kutoka nchi jirani kwa njia za panya ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege ambao unaweza kutokea wakati wanapoingiza mayai hayo.

    Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dk. Damian Kilyenyi ameeleza kuwa asilimia kubwa ya mayai yanaingizwa kwa njia za panya kutoka Rwanda, Uganda na Burundi.

    Aidha, Dk. Kilyenyi alisema mwaka jana walikamata gari likiwa na trei 700 za mayai kutoka Rwanda yenye thamani ya Sh. milioni 4.9 mali. Alisema lengo la kuzuia mayai kutoka nje kuingia nchini humo ni kupambana na ugonjwa wa mafua ya ndege, ambayo yanaweza kujitokeza kupitia kuwalisha wateja mayai ambayo asilimia kubwa ni mabovu.

    Sheria ya Chakula na Dawa ya mwaka 2018 inasema chakula chochote kinachosafirishwa bila nyaraka zinazohitajika hakifai kwa matumizi ya binadamu. Hata hivyo, alisema wafanyabiashara wanaagiza mayai hayo na kuyapitisha kwa njia za panya kutokana na kuuziwa kwa bei ndogo, na kuuza kwa bei kubwa kwa tamaa za kupata faida kubwa, huku wakijua wanahatarisha afya za watumiaji.

    Pia aliwataka kuacha tabia ya kuendelea kuingiza mayai hayo kienyeji kwa kushirikiana na wafanyabiashara kutoka nchi za jirani ili kutoendelea kuingia hasara, na badala yake waagize mayai kutoka mikoa inayofunga kuku kwa wingi nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako