• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asema kazi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona zifanywe kwa mujibu wa sheria

    (GMT+08:00) 2020-02-05 20:11:23

    Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zaidi zifanywe katika utungaji na utekelezaji wa sheria, shughuli za mahakama na kufuata sheria ili kuimarisha uwezo wa kufanikisha kazi za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vipya vya korona kwa mujibu wa sheria.

    Rais Xi ameyasema hayo leo hapa Beijing alipoendesha mkutano wa tatu wa tume ya utawala wa taifa kwa mujibu wa sheria kwa pande zote ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China. Amesisitiza kuwa, hivi sasa kazi za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi ziko katika kipindi muhimu, na ni lazima kufanya kazi hizo kwa njia ya kisayansi na kwa kufuata mpango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako