• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wayataka majeshi ya Sudan Kusini kuondoka kwenye makazi raia

    (GMT+08:00) 2020-02-06 09:24:36

    Umoja wa Afrika umelitaka jeshi la Sudan Kusini na wana usalama "kuondoka mara moja" bila masharti kutoka kwenye maeneo ya raia wanayokalia kiharamu.

    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limetoa taarifa likitaka jeshi na watumishi wa usalama kuondoka kutoka kwenye majengo 25 ya raia, na kuonya kuwa vitendo vya kushikilia majengo kama hayo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na kuendelea kupuuza mwito wa kuondoka kunaweza kusababisha kuwekewa vikwazo kwa wote wanaohusika.

    Baraza hilo limetoa mwito huo kwenye mkutano wa hivi karibuni unaofuatilia maendeleo ya hali ya Sudan Kusini. Baraza pia limeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa msukosuko wa kibinadamu nchini Sudan Kusini, na kutaka nchi wanachama kutoa msaada wa hali na mali kupunguza madhara yake kwa watu wa Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako