• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Messi ampa makavu Mkurugenzi wa Barcelona Erick Abidal kwa kuwashutumu wachezaji wa Barcelona

  (GMT+08:00) 2020-02-06 10:45:08

  Nahodha wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonyesha kukasirishwa na kauli ya Mkurugenzi wa Barcelona, Erick Abidal kwa kuwashutumu wachezaji wa Barcelona akisema kwamba walikuwa hawajitumi kwa bidii kipindi cha kochaa Ernesto Valverde. Messi amejibu kwa kumtaka Abidal atoe majina ya wachezaji hao vinginevyo anachafua jina la kila mchezaji na uvumi ambao sio kweli. Messi alitoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa Instagram akiweka kwenye Insta story akiwaambia maafisa wakuu wa Klabu hiyo kufanya majukumu yao na akawatahadharisha dhidi ya kutaja baadhi ya wachezaji wakisema kuwa hakukuwa na maelewano kwa baadhi ya watu. Amesema wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa kile kinachotokea uwanjani na huwa wako tayari kuwajibika na kutatua endapo kunakuwa na matatizo juu yao, na kwa wote ambao wanaisimamia timu wanatakiwa kuchukua maamuzi na kusimamia kile wanachokisimamia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako