• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar Airways kuwekeza RwandAir

    (GMT+08:00) 2020-02-06 19:51:59
    Iwapo vipengee vya majadiliano vitaenda kama ilivyopangwa,Shirika la ndege la Qatar Airways huenda likanunua asilimia 49 ya hisa katika shirika la ndege la RwandAir.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Qatar Airways Akbar Al Baker ,jana jumatano jijini Doha,alithibitisha kuwa Shirika hilo liko kwenye majadiliano ya kununua hisa katika Shirika la ndege la RwandAir,linalochukuliwa kuwa moja ya mashirika ya ndege yanyokua kwa kasi barani Afrika.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa RwandAir Yvonne Manzi Makolo, ambaye yuko Qatar,pia alithibitisha kuwa wako kwenye mchakato wa majadiliano lakini hakueleza mengi kuhusu mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako