• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATI yatoa mapendekezo ya kuvutia wawekezaji Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-02-06 19:52:22

    Katika mazungumzo kati yake na serikali ya Tanzania, kampuni ya uwakala wa bima ya Afrika (the African Trade Insurance Agency - ATI) imetoa mapendekezo yatakayoisaidia nchi kuvutia wawekezaji.

    Mapendekezo ya ATI pia yananuia kuisaidia nchi kupunguza gharama za kufadhili miradi ya baadaye kwa kati ya Dola za Marekani milioni 2 hadi Dola milioni 3 kwa mwaka kwa muda wa miaka kumi au zaidi.

    Tanzania ni mwanachama mwanzilishi wa ATI.

    ATI ni taasisi ya kimataifa na ya kiafrika inayojishughulisha na kutoa dhamana za uwekezaji na mikopo ili kusaidia nchi wanachama kukuza viwango vya wawekezaji.

    Katika mfumo unaopendezwa (wa credit wrap), ATI imeshazisaidia nchi kadhaa za Afrika kupata mikopo kwa riba nafuu ambapo mwaka 2019, nchi za Benin na Côte d'Ivoire zilibahatika kupata mikopo inayofikia karibu Dola bilioni 1 (zaidi ya Sh. trilioni 2.3).

    Mikopo hiyo itakuwa na riba za kiwango cha chini cha digiti moja (chini ya asilimia 10) na kulipwa kwa miaka zaidi ya 10 hadi 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako