• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Kenya Mzee Moi kuzikwa jumatano ijayo

    (GMT+08:00) 2020-02-06 19:53:57

    Rais wa pili wa Kenya, Mzee Daniel arap Moi aliyefariki dunia jumatatu asubuhi, atazikwa wiki ijayo katika shamba lake lililoko Kabaraka, kilomita 200 kaskazini magharibi mwa jiji la Nairobi.

    Mkuu wa Utumishi wa Umma nchini Kenya Joseph Kinyua amesema, mwili wa Mzee Moi utaagwa kwa heshima zote za kitaifa katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi siku ya jumanne, na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mabalozi wa nchi za nje nchini Kenya.

    Amesema serikali imetangaza siku ya jumanne kuwa siku ya mapumziko ili kuwapa wananchi nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Moi ambaye aliiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1978 hadi 2002.

    Mzee moi amefariki akiwa na umri wa miaka 95.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako