• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China amwambia mwenzake wa Marekani kuwa China ina imani na uwezo wa kushinda maambukizi ya virusi

    (GMT+08:00) 2020-02-07 15:22:30

    Rais Xi Jinping wa China amemwambia mwenzake wa Marekani Donald Trump kuwa China ina imani na uwezo wa kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona.

    Rais Xi amesema hayo alipoongea na rais Trump leo kwa njia ya simu, na pia amesema China imechukua hatua kamili na kujibu kwa haraka maambukizi hayo. Rais Xi pia amemwahakikishia mwenzake wa Marekani kuwa mustakbali wa ukuaji wa uchumi wa muda mrefu haujabadilika.

    Rais Xi ameeleza kuwa China sio tu inalinda usalama na afya ya watu wake, bali pia inalinda usalama na afya ya watu wa nchi nyingine duniani.

    Ameongeza kuwa China ikiwa imefuata mtazamo wa uwazi na kuwajibika, na kuliarifu Shirika la Afya Duniani WHO na nchi na sehemu husika ikiwemo Marekani hali ya maambukizi ya virusi, na pia imewaalika wataalam kutoka WHO na sehemu nyingine kufanya utafiti mjini Wuhan.

    Huku akikumbusha kuwa China iko mstari wa mbele wa kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo, rais Xi amesema nchi yake imechukua hatua kabambe na zenye ufanisi kwa wakati na juhudi, ambazo zimetambuliwa na kupongezwa sana na WHO na nchi nyingine. Rais Xi amesema China na Marekani zimedumisha mawasiliano katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, na amepongeza kauli nzuri za rais Trump kuhusu juhudi za China katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, na kuwashukuru watu wa hali mbalimbali katika jamii ya Marekani kutokana na misaada yao.

    Rais Xi amesema kwa sasa kazi ya kudhibiti maambukizi iko katika kipindi muhimu, na ametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ugonjwa huo wa kuambukiza, akisisitiza kutochukua hatua kupita kiasi kama ilivyosisitiza WHO.

    Rais Xi amemwambia Trump kuwa China inatarajia Marekani kutathmini hali ya maambukizi hayo kwa usahihi na utulivu, na kurekebisha hatua zake za kuyajibu.

    Kwa upande wake, rais Trump amesema Marekani inaunga mkono kikamilifu juhudi za China za kupambana na ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na virusi vipya vya korona, na inapenda kupeleka wataalam China ili kuisaidia nchi hiyo kwa njia mbalimbali.

    Rais Trump ameeleza kuwa China inastahili kupongezwa kwa kujenga hospitali za muda ndani ya muda mfupi, jambo ambalo limeonesha mpango na uwezo mzuri wa China. Ameongeza kuwa anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Xi, watu wa China hakika wataweza kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi.

    Rais Trump pia amesema Marekani ina imani na maendeleo ya uchumi wa China, na kwamba Marekani itachukua mtazamo wa utulivu katika kujibu maambukizi hayo, pia inapenda kudumisha mawasiliano na ushirikiano na China kati ya pande hizo mbili na WHO.

    Wakati huohuo, rais Xi amesisitiza kuwa kusainiwa kwa makubaliano ya kiuchumi na kibiashara ya kipindi cha kwanza sio tu kunanufaisha nchi hizo mbili, bali pia kunalinda amani na ustawi wa dunia.

    Amesema hii imeonesha wazi kuwa licha ya tofauti mbalimbali kati ya China na Marekani, iwapo pande hizo mbili zitatendeana kwa usawa na kuheshimiana, zinaweza kupata suluhu inayokubaliwa kwa pande zote kupitia mazungumzo na mashauriano.

    Rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa Marekani na China zinaweza kushirikiana na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa, kushikilia kanuni za kimsingi za uratibu, ushirikiano na utulivu, na kuhimiza uhusiano wa pande mbili uelekee kwenye njia ya sahihi katika mwaka huu mpya.

    Naye rais Trump amesema Marekani inapenda kushirikiana na China kutekeleza makubaliano hayo na kufanya juhudi kwa pamoja kukuza uhusiano wa nchi hizo.

    Marais hao wawili pia wamekubaliana kudumisha mawasiliano ya karibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako