• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahojiano na Albert M.Muchaga, Kamishna wa Viwanda na Biashara iliyo chini ya Kamati ya Umoja wa Afrika

  (GMT+08:00) 2020-02-07 18:10:48

  Swali: Mapema mwaka huu, Marekani na China zilisaini makubaliano ya kibiashaa yaliyoondoa mvutano kati ya nchi hizo mbili kubwa duniani kiuchumi. Unadhani kuna umuhimu gani wa kusaini makubaliano hayo kwa uchumi wa dunia, biashara, uwekezaji na soko la fedha?

  Jibu: "Nadhani wakati naongea na wanahabari nilidokeza umuhimu wa kusuluhisha migogoro katika kurahisisha mtiririko wa biashara kati ya nchi na nchi na katika nchi. Hivyo chanzo cha makubaliano hayo ya kibiashara ni kwamba, kulikuwa na ushuru unaoibuka ambao haukuweza kuwa rasmi, hivyo wanaelekea kwenye makubaliano, ambalo ni jambo zuri. Ina maana kuwa kuna makubaliano ya pamoja, na hilo linakwenda kurahisisha mtiririko wa biashara duniani, nah ii ni hatua nzuri ambapo sisi hapa Afrika tunaipongeza"

  Swali: Kuna umuhimu gani kivitendo kwa Afrika kutokana na uzoefu wa China katika maendeleo yenye ubora wa juu, kuboresha viwanda, uvumbuzi wa kiteknolojia na nyanja nyingine?

  Jibu: "Kampuni nyingi za China zinawekeza katika mambo ya asili barani Afrika na zinashiriki katika mageuzi ya kiviwanda ya Afrika ambayo tunafanya kila mwaka. Novemba mwaka jana tulifanya maonyesho yaliyofana sana katika ukumbi huu, kwa ushirikiano na Kituo cha Kimataifa cha Biashara na serikali ya Ethiopia. Hivyo, uwekezaji wa China, kama uwekezaji wengine kutoka duniani unakaribishwa, na wanajitangaza vizuri sana barani Afrika."

  Swali: Wakati Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika linatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa, unatarajia nini katika ushirikiano huo kwa Afrika hususan katika sekta ya Biashara na Viwanda?

  Jibu: "Sasa msingi wa wenzi wa ushirikiano kati ya China na Afrika ni ushirikiano wa kunufaishana. Umesisitizwa sana na wakuu wa nchi na serikali, akiwemo rais wa China. Hivyo tunapoelekea kwenye miaka mingine 20, tunatarajia kuendelea kwa ushirikiano katika msingi wa kunufaishana kati ya vuongozi na kati ya wenzi wa masoko na watu wa kawaida. Hivyo ni mfumo mzusi sana wa ushirikiano wa maendeleo, na tunafikiri kuwa utaendelea kukua katika miaka ijayo."

  "Viwanda ni kitu kikubwa, kikubwa sana, lakini ukiangalia mahitaji ya Waafrika, wanahitaji vyakula vilivyotengenezwa ili wavihifadhi kwa muda mrefu zaidi, wanahitaji viatu, wanahitaji nguo, wanahitaji makazi, na wanahitaji mambo mengine yanayohusiana na viwanda. Binadamu ana mahitaji mengi sana. Nikikuangalia wewe, unahitaji kunyoa nywele, unahitaji kupaka mafuta, unahitaji nguo, unahitaji saa, unahitaji kumnunukua mpoenzi wako…. hivyo, kuna mahitaji mengi. Sasa tusijaribu kusema moja mbili moja mbili hapana, hatutakuwa tunafanya kazi nzuri. Tuweke wazi kuwa mfumo wa ushirikiano wa mageuzi ya kiviwanda kati ya China na Afrika umeanzishwa na unatarajiwa kukua."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako