• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshambuliaji auawa baada ya kuwaua watu 27 Thailand

    (GMT+08:00) 2020-02-09 17:27:44

    Mshambuliaji aliyewaua watu 27 na kuwajeruhi wengine 57 kwenye tukio kubwa la ufyatuliaji risasi ovyo lililotokea kaskazini mashariki mwa Thailand ameuawa na polisi leo asubuhi.

    Jenerali mkuu wa polisi Chakthip Chaijinda amesema mwanamume huyu aliyesheheni silaha na kutambuliwa kuwa Sajenti Jakrapanth Thomman aliuawa katika jengo la maduka la Terminal 21 baada ya saa karibu 18 za ufyatuliaji risasa na kupambana na polisi. Mwanajeshi huyo alitoka kambi ya kijeshi ya Suratham Phithak mkoani Nakhon Ratchasima, kilomita 160 kaskazini mashariki ya Bangkok.

    Habari zinasema Sajenti huyo alikuwa na mzozo kuhusu mkataba wa ardhi na maofisa wa jeshi na mwanamke mmoja aliyemwua kwa risasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako