• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu mwenyekiti wa AU aunga mkono ndugu wa China katika kupambana na virusi vipya vya korona.

    (GMT+08:00) 2020-02-09 18:06:14

    Mkutano wa 33 wa wakuu wa Umoja wa Afrika umefunguliwa leo mjini Addis Ababa, Ethiopia. Naibu mwenyekiti wa umoja huo Bw. Thomas Kwesi Quartey alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kabla ya mkutano huo, amesifu juhudi za China katika kupambana na virusi vipya vya korona, na kusema Umoja wa Afrika unaiunga mkono China kwenye mapambano hayo.   

    "Ningependa pia kutumia fursa hii kuwaambia ndugu zetu wachina kuwa mshikamano wetu wakati huu wa athari mbaya za virusi vya Korona, na tunavutiwa sana na jinsi China inavyohamasisha vifaa na raslimali za teknolojia na sayansi katika kushughulikia suala hili. Tunapenda sana kuendelea na ushirikiano huu na China, sisi tunaiunga mkono China na China inatuunga mkono."

    Alipozungumzia mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika, amefahamisha kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni "kuacha bunduki: kuanzisha mazingira mazuri kwa maendeleo ya Afrika", na kwamba mkutano huo utajadili mada kuhusu amani na usalama wa Afrika. Anaona kuwa China inatoa mchango mkubwa katika kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, na uzoefu wa China unastahili kuigwa na nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako