• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi apongeza kufunguliwa kwa mkutano wa 33 wa wakuu wa Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-09 19:53:53

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mkutano wa 33 wa wakuu wa Umoja wa Afrika unaofunguliwa leo Addis Ababa, Ethiopia.

    Rais Xi amesema toka mwaka jana, chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika, nchi za Afrika zimejitahidi kutafuta njia za maendeleo kulingana na hali zao halisi, kushikilia kutatua matatizo ya Afrika kwa mtindo wa kiafrika, na kuzindua rasmi eneo la biashara huria la Afrika. Afrika imepata maendeleo madhubuti kwa kushikiriana, na nguvu yake ya ushawishi kuimarika ulimwenguni.

    Rais Xi ameongeza kuwa wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajashuhudiwa katika miaka 100 iliyopita, kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika iliyo na uhusiano wa karibu zaidi kunaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Amessisitiza kuwa China itaendelea kuzitendea nchi za Afrika kwa udhati, urafiki, na kuhimiza ushirikiano wao uzae matunda halisi, na kuangalia haki na maslahi kwa mtazamo sahihi, kuhimiza kwa pande zote makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, kuharakisha ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya Afrika na kuwanufaisha watu wa China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako