• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN na AU zaendelea kuiunga mkono China kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya Korona

    (GMT+08:00) 2020-02-10 09:40:37

    Kwenye mkutano wa kilele wa 33 wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wameeleza kuiunga mkono China kupambana na mlipuko wa virusi vya Korona, na kutetea kuzuia lugha mbaya na kueneza uvumi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, China imefanya juhudi kadiri iwezavyo kuzuia kuenea kwa maambukizi kazi ambayo si rahisi, jumuiya ya kimataifa inapaswa kushikamana na kushirikiana kupambana na mlipuko wa virusi hivyo. Pia amesema inapaswa kutoinyanyapaa na kuishambulia China.

    Mwenyekiti wa mkutano wa 74 wa baraza la 4 la Umoja wa Mataifa Bw. Mohammed Bandi amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kushikamana na kushirikiana, na kuzuia uvumi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona. Pia amepongeza hatua za China za kutangaza habari kuhusu mlipuko wa virusi hivyo.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema Afrika iko pamoja na ndugu wa China kupambana na virusi vipya vya Korona. Baraza tendaji la Umoja wa Afrika limetoa taarifa likisema mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanaiunga mkono China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako