• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini atoa wito wa umoja katika kukabiliana na changamoto

    (GMT+08:00) 2020-02-10 19:46:21

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametumia maadhimisho ya miaka 30 tangu Nelson Mandela kuachiliwa huru kutoka jela kuitaka nchi hiyo kuwa na umoja katika kukabiliana na changamoto.

    Akizungumza siku moja kabla ya nchi hiyo kuadhimisha miaka 30 tangu Nelson Mandela aachiwe huru, rais Ramaphosa amesema ukosefu wa usawa, ajira, umasikini na vurugu vimeendelea kuwa changamoto kubwa kwa nchi hiyo, miaka 30 baada ya Mandela kuachiwa huru.

    Mandela aliachiliwa huru kutoka gerezani Februari 11, 1990, katika hatua ya kihistoria ya safari ya Afrika Kusini kuelekea kwenye demokrasia, ambayo ilitimizwa miaka minne baadaye.

    Amesema nchi hiyo inatafuta ukuaji, uchumi jumuishi ambao unatoa nafasi za ajira, nchi yenye uwezo wa maendeleo inayotoa huduma za gharama nafuu kwa ufanisi, na upatikanaji wa elimu, afya, makazi, na usalama kwa wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako