• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaipa Afrika vifaa 3,000 vya kupima virusi vya korona

  (GMT+08:00) 2020-02-11 09:49:11

  China inaendelea kutoa msaada kwa Afrika ili kuitayarisha kukabili virusi vya korona ikiwa vitatokea barani humo.

  Wiki hii vifaa 3,000 vya kupima virusi hivyo vinawasili kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika kutoka china ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kukabili vurusi hivyo.

  Ronald Mutie anaripoti kutoka Ethiopia.

  Bado hakuna tukio lolote la maambukizi ya virusi vya korona barani Afrika.

  Lakini serikali, mashirika ya ndege na taasisi za afya barani humo zimechukua hatua mbali mbali ili kuvikabili virusi hivyo iwapo vitatokea.

  Na juhudi hizo pia zinaungwa mkono na China kupitia utoaji habari husina na vifaa.

  Mkurungezi wa kituo cha kupambana na magonjwa barani Afrika bwana John Nkengasong anasema sasa Afrika imeimarisha hata zaidi utayari wake wa kupiga vita korona.

  "China tayari imetupatia vifaa 3,000 vya kufanya upimaji na tutaziifadhi na kuzitumia ikiwa kutakuwa na dharura . kwa hivyo katika upande wa kufanya upimaji na utambuzi tuko tayarizaidi hata kuliko tulivyokuwa wiki iliopita. Wiki hii pia tumewapa mafunzo wafanya kazi wa shirika la ndege la Ethiopia na taasisi ya afya ya uma ya Ethiopia ili kuhakikisha wamejiandaa kukabili hali yoyote. Tutaongeza utoaji wa mafunzo kama hayo kwa mashirika zaidi ya ndege na wiki hii tutakuwa na zoezi kama hilo nchini Kenya kwa kushirikisha mashirika ya Afrika. Hivyo tunapiga hatua za haraka iwezekanavyo kuandaa Afrika ikiwa kutakuwa na mplipuko"

  Nchini china wenyeji wameanza kurejea kazini baada ya kurefushwa kwa sikukuu ya mwaka mpya wa kichina ili kupunguza uwezekano wa kusambaa kwa aina hiyo mpya ya virusi.

  Tangu kunguduliwa kwa virui hivyo serikali na taasisi zote za matibabu nchini china zilifanya juhudi za haraka kuvitambua na kuanza mara moja katibabu kwa waadhiriwa lakini pia kupunguza maambukizi mapya.

  Juhudi hizo ni pamoja na ujenzi wa hospitali kubwa ya zaidi ya vitanda 1,000, kunyunyiza dawa na kutoa habari.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana António Guterres anapongeza juhudi za china huku akitaja virusi hivyo kuwa janga la kimataifa.

  "Ni wazi kuwa kuna juhudi kubwa ambayo inafanywa na China ili kukabili ugonjwa huo na kuepusha kuenea kwake. Na nadhani kwamba juhudi hiyo tayari ni kubwa. Wachina wenyewe wanagundua kuwa kuna mapungufu na shida kadhaa ambazo zinapaswa kushughulikiwa, lakini pia wakati huo huo tumejitolea kupitia Shirika la Afya duniani kuunga mkono nchi zote, zikiwemo nchi za Kiafrika, ili kukuza uwezo wa kukabili ugonjwa huo wakati ukienea kwa nchi zingine ulimwenguni. Nadhani hii ni hali mbaya ya janga ambayo inahitaji ushirikiano wenye nguvu sana wa kimataifa na mshikamano."

  Barani Afrika serikali zinajiandaa kwa kuanzisha taasisi kubwa za kupambana na magonjwa na pia utengenezaji na ukaguzi wa madawa.

  Tayari serikali ya China ilitoa dola milioni 80 kusaidia ujenzi wa kituo cha kupambana na magonjwa cha Afrika kitakachojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

  Na ili kuongeza uwezo wa kujitegema na madawa Umoja wa Afriak pia unaanzisha shirika la dawa la Afrika.

  Kamishena wa maswla ya jamii katika umoja wa Afrika Bibi Amira El Fadil anaeleza.

  "Shirika hilo litakuwa la kuthibiti madawa yanayotengezwa barani Afrika, na ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya kutengeneza madawa Afrika. Pia shirika hilo litakuwa na jukumu la kusaidia kujenga uwezo katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika . Litafanya kazi za kuunganisha sera kwenye sekta ya utengenezaji madawa na kulinda Afrika dhidi ya madawa yasiofikia viwango kuingia humo"

  Shirika hilo litajengwa baada ya nchi zote kukubaliana kuhusu nchi kitakapokuwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako