• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Robert Farah kutofungiwa kucheza tenisi licha ya vipimo vyake kuonekana anatumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni

    (GMT+08:00) 2020-02-11 11:18:22

    Bingwa wa Wimbledon na Michuano ya wazi ya Marekani kwa wachezaji wawiliwawili Robert Farah, hatafungiwa kucheza tenisi licha ya vipimo vyake kuonesha anatumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni na kukiuka mpango wa kupambana na dawa hizo. Mcolombia huyo mwenye miaka 33, awali alifungiwa kwa miezi mitatu baada ya kuonekana anatumia dawa hizo. Farah amesema uwepo wa anabolic steroid Boldenone unatokana na kula nyama iliyochafuliwa nchini kwao. Shirikisho la Tenisi Kimataifa (ITF) limemkubalia Farah kuwa hana hatia ya kukiuka mpango huo. Matokeo hayo yalitoka mwezi Oktoba na Farah kuthibitishiwa na ITF mwezi uliopita jambo lililomfanya akose michuano ya Australian Open.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako