• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yahimiza kudhibiti maambukizi ya virusi vipya vya korona kwa njia ya kisayansi

  (GMT+08:00) 2020-02-11 17:32:10

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus amesema, shirika hilo linachukua hatua mbalimbali kuratibu nguvu za kisayansi duniani, ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kwa njia ya kisayansi. Aidha amehimiza kuongezwa kwa ushirkiano wa kimataifa.

  Akizungumza na wanahabari jana mjini Geneva, Bw. Ghebreyesus amesema maambukizi ya virusi vipya vya korona bado hayajapungua. Anasema,

  "Hali ya jumla ya maambukizi hayo bado haijabadilika. Asilimia 99 ya kesi za maambukizi hayo zinatoka China, wagonjwa wengi wana hali nzuri, na kiwango cha kifo ni karibu asilimia 2. Kiwango hicho bado ni kikubwa."

  Hivi sasa watu wengi wanafuatilia zaidi mwelekeo wa maambukizi hayo, na kutaka kujua utakuwa mzuri au mbaya zaidi. Mkurugenzi huyo amesema, hata WHO inafanya juhudi ili kutafuta majibu.

  "Ili kujibu maswali hayo, tunafanya kazi mbalimbali. Kwanza, Kongamano la Kimataifa la Utafiti na Uvumbuzi litanza tarehe 11, ili kujadili baadhi ya maswali hayo, na kuweka wazi hatua zinazopasa katika siku zijazo. Pili, ujumbe wa wataalamu wa WHO unaoongozwa na Dr. Bruce Aylward umefika nchini China, ili kuweka msingi wa kupanua timu ya kimataifa."

  Kongamano la Kimataifa la Utafiti wa Uvumbuzi unaolenga virusi vipya vya korona litafanyika leo na kesho mjini Geneva. Kongamano hilo litashirikisha wanasayansi bingwa duniani na wataalamu wa idara za afya na utafiti za nchi mbalimbali. Mada tisa zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na umaalumu wa virusi, chanzo chake, uchunguzi wa maambukizi, na matibabu na chanjo, ili kuratibu nguvu za kisayansi duniani, kuamua mambo ya utafiti yatakayowekewa kipaumbele, kutafuta mpango bora zaidi wa matibabu, na kutafiti chanjo.

  Ikilinganishwa na hatua nyingine, Tedros amesisitiza kuwa WHO inajitahidi kufanya maabara ziwe na uwezo wa kuthibitisha maambukizi haraka. Amesema zuwezo huo ukikosekana, nchi mbalimbali duniani hazitaweza kugundua maambukizi ya virusi vipya ya korona na maambukizi mengine yanayofanana, na pia zitashindwa kujua upana na kina cha maambukizi hayo. Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na maambukizi hayo. Anasema,

  "Lengo letu bado ni kuzuia maambukizi, nataka nchi zote duniani zizingatie fursa ya hivi sasa ya kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo. WHO litaendelea kushirikiana na nchi hizo kukinga na kugundua kesi mpya za maambukizi hayo, ili kuokoa maisha ya watu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako