Katibu mkuu wa idara ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona iliyo chini ya Baraza la Serikali la China Bw. Cong Liang amesema sekta muhimu zinazohusiana na uchumi wa taifa na mahitaji ya watu zinapaswa kurudisha uzalishaji mara moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hapa Beijing, Bw. Cong pia amesema miradi mikubwa inapaswa kuanzishwa mapema iwezakanavyo, na sehemu zinazokumbwa na hali mbaya ya maambukizi na sekta zisizokuwa za lazima zinaweza kuahirisha uzalishaji.
Hivi sasa, mikoa mbalimbali kando ya mkoa wa Hubei inarejesha uzalishaji hatua kwa hatua, hasa sekta muhimu zikiwemo raslimali ya matibabu, nishati, vyakula, mawasiliano na usafirishaji wa bidhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |