• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu milioni 22 nchini Marekani waambukizwa virusi vya mafua kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana hadi sasa

  (GMT+08:00) 2020-02-11 17:55:11

  Takwimu mpya kutoka Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa nchini Marekani zimeonesha kuwa, kuanzia tarehe 29 mwezi Septemba mwaka jana, watu milioni 22 nchini humo waliambukizwa virusi vya mafua, miongoni mwao watu laki 2.1 walipata matibabu hospitalini na wengine 12,000 walifariki.

  Takwimu nyingine za awali za kituo hicho pia zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2010, watu milioni 9 hadi milioni 45 waliambukizwa virusi vya mafua kila mwaka nchini Marekani, na watu kati ya 12,000 hadi 61,000 walifariki kutokana na ugonjwa huo.

  Kituo hicho kimesema, kupata chanjo ya virusi vya mafua ni njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa huo na magonjwa mwengine makali yanayosababishwa na virusi hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako