Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga kufanya mkutano leo kujadili mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Marekani.
Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema, katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres na mjumbe maalum wa mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati wa Umoja wa Mataifa Bw. Nickolay Mladenov watatoa hotuba kwenye mkutano huo. Rais Mahmoud Abbas wa Palestina pia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |