• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tundo afungua mwanya wa alama tano katika mbio za magari Kenya

  (GMT+08:00) 2020-02-11 18:06:39

  Dereva wa mbio za magari nchini Kenya Carl "Flash" Tundo amechukua uongozi wa mapema wa Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) 2020, baada ya kujizolea alama 25 kwa kushinda duru ya ufunguzi ya KCB Guru Nanak katika maeneo ya Stoni Athi, Jumapili. Katika mfumo mpya wa kuwapatia washiriki pointi, Tundo, ambaye alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa Guru Nanak kwa mara ya pili mfululizo, aliongezwa alama tatu za ziada. Baldev Chager, ambaye aliibuka mfalme wa mbio za magari nchini Kenya mwaka 2019, alikusanya alama 21 kwa kumaliza nyuma ya Tundo. Chager pia alitunukiwa alama mbili za ziada na sasa ana jumla ya alama 23. Onkar Rai anakamilisha orodha ya madereva tatu-bora waliopokea alama za ziada kwa kutia kapuni alama 18 kwa kukamilisha Guru Nanak katika nafasi ya tatu na kuambulia alama moja ya bonasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako