Idara ya afya ya mkoa wa Hubei, nchini China leo imeripoti kuwa, mpaka kufikia jana, idadi ya kesi mpya za maambukizi ya virusi vipya vya korona imekuwa 2,097, na watu 103 wamefariki jana kutokana na ugonjwa huo.
Ripoti hiyo imesema, idadi hiyo ni ya chini zaidi katika siku 9 zilizopita. Tarehe Mosi mwezi huu, idadi ya kesi mpya za maambukizi hayo mkoani Hubei ilikuwa 1,921, na idadi hiyo ilikuwa zaidi ya 2,100 kwa siku mpaka kufikia jana. Wagonjwa 427 waliruhusiwa kuondoka hospitali hapo jana baada ya kupona, na hadi jana idadi ya jumla ya wagonjwa waliopona na kutoka hospitali imefikia 2,222 mkoani humo.
Wakati huohuo, Ofisa wa Kamati ya afya ya China Bw. He Qinghua amesema, idadi ya kesi mpya za maambukizi ya virusi vipya vya korona imepungua kwa siku saba mfululizo nje ya mkoa wa Hubei nchini China,.
Ameongeza kuwa hatua zinazochukuliwa na serikali ya China zimefanya kazi muhimu katika kuzuia virusi vipya vya korona, ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kupendekeza kutosafiri katika wakati mmoja, na kuimarisha usimamizi wa usarifi wa watu walioko katika maeneo ya hali mbaya ya maambukizi hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |