• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali kupata shilingi bilioni tano kwa kuuza vyumba kwa raia

  (GMT+08:00) 2020-02-11 18:44:57
  Serikali ya kitaifa inatarajia kupokea takriban shilingi bilioni tano kutoka kwa mauzo ya nyumba 1,370, za bei nafuu. Ikumbukwe kwamba moja wapo ya ajenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta, ni wakenya kupata nyumba kwa bei nafuu. Nyumba hizi zinaendelea kujengwa katika maeneo ya Nairobi, Embu, Machakos, Kiambu na Kisumu.

  Kulingana na bei rasmi, nyumba yenye chumba kimoja cha kulala katika eneo la Nairobi, itauzwa kwa shilingi milioni 1.5. Nyumba yenye vyumba viwili vya kulala itauzwa kati ya shilingi milioni mbili na tatu. Nyumba ya vyumba vitatu vya malazi itauzwa kwa shilingi milioni 3.5 hadi 4. Kuna nyumba 548 ambazo zinajengwa Nairobi.

  Watakaopewa kipao mbele, ni wafanyikazi wa serikali ambao makazi yao yalibomolewa ili kujenga vyumba hizi za serikali.

  Katika kaunti ya Embu, serikali inajenga nyumba 220, ambako nyumba yenye vyumba viwili vya kulala itauzwa kwa shilingi milioni 3.5.

  Kaunti ya Machakos, serikali inajenga nyumba 200, ambako nyumba ya vyumba viwili vya kulala, itauzwa kwa shilingi milioni 3.3.

  Kaunti ya Kiambu, ni nyumba 193 zinazoendelea kujengwa na Kisumu ikiwa na nyumba 210.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako