• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wachina waanza kurejea kazini

  (GMT+08:00) 2020-02-11 18:45:32
  Serikali ya China imeanza kulegeza sheria kwa raia wake baada ya mkurupuko wa virusi vya Corona, ambavyo vimesababisha vifoo vya mamia ya wachina na kuwaathiri maelfu kadhaa. Wafanyikazi nchini humo wameanza kurejea kazini na baadhi ya viwanda kuanza oparesheni zao.

  China ilikuwa imeweka sheria kali kwa raia wake ya kutotangamana au hata kutoka nje kama njia moja ya kukabili virusi hivi. Biashara nyingi zilifungwa na hivyo kuathirika pakubwa tangu kugunduliwa kwa virusi hivi vya Korona.

  Shirika la Afya Duniani WHO limetuma wataalam wa afya kwenda Beijing kuchunguza hali halisi ya virusi hivi.

  Kumekuwa na hofu kwamba kuendelea kufungwa kwa kampuni na viwanda nchini China, ambayo ni ya pili ulimwenguni kwa ukubwa kiuchumi, kungeathiri uchumi wa mataifa mengi duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako