• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nzige wa jangwani wavamia Uganda

  (GMT+08:00) 2020-02-11 18:47:23
  Uganda imethibitisha uvamizi wa nzige wa jangwani katika eneo la Karamoja lililo mashariki mwa nchi hiyo.

  Kundi la kwanza la nzige lilionekana saa tisa mchana siku ya Jumapili katika wilaya ya Moroto.

  Makundi mawili ya wadudu hao waharibifu yamegunduliwa eneo la Karamoja nchini Uganda.

  Serikali ikishirikisha majeshi imewapeleka makundi ya maofisa na wataalamu kupambana na nzige hao.

  Katika muda wa saa tatu tu baada ya nzige hao kuonekana mpakani, walikuwa wamefika katika wilaya mbili jirani za Amudat na Nakapiripirit.

  Kundi hilo la nzige linadhaniwa lilitokea eneo la Pokot Magharibi nchini Kenya.

  Kwa kuwa nzige hao wanasambaa kwa kasi kubwa, maafisa wa wizara ya kilimo wanasema watalazimika kusambaza vifaa maeneo mbalimbali ili kukabiliana nao.

  Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimeathiriwa na uvamizi wa nzige hao ni Kenya, Somalia na Ethiopia

  Kulingana na shirika la chakula na kilimo duniani uvamizi huu wa nzige ndiyo mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 70.

  Kundi moja la nzige laweza kuharibu chakula cha hadi watu 2,500 kwa siku moja tu, na hujumuisha wadudu milioni 150 katika eneo la kilomia moja mraba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako