• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Imani, nia na hatua za China kupambana na maambukizi zaimarishwa zaidi

  (GMT+08:00) 2020-02-11 21:10:38

  Rais Xi Jinping wa China jana mjini Beijing alipokagua kazi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona amesisitiza kuwa, hivi sasa hali ya maambukizi hayo bado ni ya wasiwasi sana, na China inapaswa kuimarisha imani, nia na hatua, na kutegemea wananchi kwa karibu, ili kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo, na kushinda vita dhidi ya virusi.

  Tahariri iliyotolewa na Shirika Kuu la Utangazaji la China yenye kichwa "Imani, nia na hatua za China kupambana na maambukizi zaimarishwa zaidi" inasema, nia imara ni muhimu zaidi kwa wananchi wa China kushinda vita dhidi ya maambukizi. Nia hiyo inatokana na mfumo hodari wa kisiasa wa China. Baada ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vipya vya korona, rais wa China amepanga na kuongoza mwenyewe hatua za kukabiliana na maambukizi hayo, ambazo zimepata ufanisi hatua kwa hatua.

  Takwimu zilizotolewa na Kamati Kuu ya Afya ya China zinaonesha kuwa, kesi mpya za maambukizi zilizotokea jana katika sehemu zote za China isipokuwa mkoa wa Hubei zilikuwa 381, na kupungua kwa siku saba mfululizo. Wakati huohuo, idadi ya wagonjwa waliopona imeongezeka kidhahiri. Hali hii inaonesha kuwa, hatua zilizochukuliwa na China dhidi ya maambukizi hayo ni za kisayansi na zenye ufanisi.

  Hivi sasa vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona imeingia katika kipindi muhimu, na hali mpya zinatokea mara kwa mara. Utambuzi, ufahamu na matibabu ya ugonjwa mpya ni mchakato wa hatua kwa hatua, na wakati huohuo, kwa kuwa Wachina wameanza kazi baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, hali ya maambukizi inatatanisha zaidi. Hivyo China inapaswa kuimarisha zaidi nia na moyo wa kushinda virusi.

  Kupambana na maambukizi ni vita ngumu ya kulinda maisha na afya ya watu. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza China kwa kufanya juhudi kubwa ili kudhibiti maambukizi na kuyazuia yasienee zaidi, akisema juhudi hizo ni za ajabu. Katika wakati huo muhimu, rais Xi kukagua kazi ya kukabiliana na maambukizi na kutoa maamuzi muhimu ni juhudi mpya ya China ya kulinda wananchi wake na watu wa dunia nzima.

  "Virusi ni zimwi, na hatuwezi kuruhusu zimwi ajifiche". Chini ya uongozi wa serikali kuu, idara husika mbalimbali za China zinafanya kazi kwa makini. China ikiimarisha imani, mshikamano, kukabiliana na maambukizi kwa njia ya kisayansi, kutegemea wananchi kwa karibu, na kuimarisha ushirikiano na jumuiya ya kimataifa, hakika itaangamiza "zimwi", na kushinda vita dhidi ya maambukizi ya virusi vipya vya korona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako