• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pele ajisikia aibu kuondoka nyumbani kwake kwasababu ya afya yake kuzorota

    (GMT+08:00) 2020-02-12 09:36:49

    Mchezaji maarufu wa soka nchini Brazil na ulimwenguni Pele hayuko radhi kuondoka nyumbani kwake kwasababu hawezi kutembea bila usaidizi. Bingwa huyo mara tatu wa kombe la dunia, aliyejipatia sifa za kuwa mchezaji bora zaidi wa soka alipelekwa hospitalini akiugua maambukizi ya mkojo mwaka uliopita. Pele mwenye umri wa miaka 79 amekuwa na tatizo la nyonga yake kwa muda mrefu na sasa anahitaji magongo ili kumsaidia kutembea huku shughuli zake nyingi za umma akizifanya akiwa katika kiti cha magurudumu. Pele alifunga jumla ya magoli 1,281 ikiwa ni rekodi ya duniani katika mechi 1,363 wakati wa kipindi chake cha miaka 21 katika kandanda, ikiwemo magoli 77 katika mechi 91 akiichezea Brazil. Hali yake ya kiafya imekuwa ikitia watu wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni na alifanyiwa upasuaji wa tezi dume 2015 baada ya kulazwa hospitalini kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi sita. Mwezi Juni ataadhimisha miaka 50 tangu ashiriki katika kombe la dunia ambalo alishinda nchini Mexico na kile kilichoaminika na wengi kuwa timu bora zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako