• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Abbas akataa mpango uliotolewa na Marekani kuhusu amani ya Mashariki ya Kati kwenye mkutano wa Baraza la usalama

  (GMT+08:00) 2020-02-12 09:42:46

  Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesisitiza kukataa mpango uliotolewa karibuni na Marekani kuhusu amani ya Mashariki ya Kati, ambao ameuita "Pendekezo la Israel na Marekani".

  Kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa unaojadili mpango huo wa Marekani, rais Abbas amesema mpango huo umekiuka sheria ya kimataifa na Mpango wa Amani wa Kiarabu.

  Rais Abbas amesisitiza kuwa mpango wa Marekani umefuta uhalali wa haki za Wapalestina, ambazo ni pamoja na haki ya kujitawala na uhuru katika nchi yao yenyewe. Pia umehalalisha vitendo haramu ambavyo ni pamoja na kuweka makazi na kunyang'anya ardhi ya Palestina.

  Habari nyingine zimesema mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov ametoa mwito wa kutafakari njia ya kuzihimiza Israel na Palestina zirudi kwenye mazungumzo, kwani mpango uliotolewa na Marekani umekataliwa na nchi za kiarabu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako