Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema kikosi cha polisi cha nchi hiyo kimewaua magaidi 17 katika mapigano yaliyotokea katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini humo. Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema, idara ya usalama ya taifa imepata habari kuhusu maficho ya kundi la kigaidi kilichoko katika eneo la al-Obaidat mjini Arish. Katika mapigano hayo silaha na nabomu pia vilikamatwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |