• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping azungumza na wenzake wa Qatar na Indonesia kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2020-02-12 09:57:34

  Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Emir wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani kwa njia ya simu.

  Kwenye mazungumzo yao Rais Xi amesisitiza kuwa wananchi wote wa China wamefanya juhudi kwa pamoja tangu maambukizi ya virusi vya korona yalipuke, ambao wamechukua hatua kali zaidi ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. Amesema kwa sasa kazi ya kupambana na maambukizi hayo inaanza kupata matokeo mazuri. China ina imani na uwezo wa kushinda vita dhidi ya virusi hivyo kutokana na mshikamano na dhamira ya wananchi, nguvu bora ya kimfumo na msingi imara wa kiraslimali na kiteknolojia, pamoja na uzoefu mkubwa.

  Wakati huohuo rais Xi Jinping jana amezungumza na mwenzake wa Indonesia Joko Widodo kwa njia ya simu, na kusisitiza kuwa China ina uwezo na imani ya kuhakikisha kushinda mapambano dhidi ya virusi vya korona, na pia itatimiza malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama ilivyopangwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako