• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa China ahimiza Baraza la Usalama kuweka mpango wa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan

  (GMT+08:00) 2020-02-12 10:01:08

  Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Wu Haitao amelitaka Baraza la Usalama kukagua hatua za vikwazo dhidi ya Sudan kwa wakati, na kuweka mpango wa kuondoa vikwazo hivyo kwa mujibu wa maendeleo mapya yanayopatikana.

  Balozi Wu amesema China siku zote inaunga mkono mchakato wa amani ya Darfur ya Sudan, na inakaribisha kupitishwa kwa azimio No. 2508 linalopanga kupitia hatua za vikwazo hivyo kila baada ya muda. Pia ameongeza kuwa vikwazo si matokeo ya mwisho, bali ni njia inayopaswa kutumiwa katika kufumbua masuala ya kisiasa.

  Siku hiyo balozi Wu pia amesisitiza kuwa hali ya jumla huko Darfur ni tulivu, na iko katika kipindi muhimu cha mpito. Amelitaka Baraza la Usalama na jumuiya ya kimataifa watambue vya kutosha juhudi zilizofanywa na serikali ya Sudan na kuheshimu uongozi wake katika suala la Darfur.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako