Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi yake haitarudi nyuma licha ya vikwazo vilivyowekwa na Marekani.
Akilihutubia taifa hilo kupitia televisheni, rais Rouhani amesema, Iran inakabiliwa na vikwazo vikali kutoka Marekani, ambayo inataka kupunguza nguvu ya Iran kwa kuongeza vikwazo zaidi katika miezi 20 iliyopita. Amesema Marekani pia inaitaka serikali ya Iran na watu wake warudi nyuma kwa kuiwekea Iran shinikizo, lakini serikali ya Iran na watu wake kamwe hawatashindwa na shinikizo hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |